
Mtaalam wa tiba asili na virutubishi tiba, Abdallah Mandai amesema mafuta ya ufuta ni tiba anuwai ya kidonda kilichosababishwa na moto.
Mandai amefichua siri hiyo leo Jumanne Septemba 13, 2022 jijini Dar es Salaam.
“Chukua mafuta ya ufuta changanya na maji ya ndimu kiasi sawa na mafuta hayo, paka sehemu iliyoungua. Fanya hivyo kila unapoosha kidonda hadi kitakapo pona.
“Mafuta ya ufuta pia yanasaidia kupunguza maumivu ya misuli kabla na baada ya mazoezi. Baada ya mazoezi oga kisha paka mwilini mafuta ya kutosha yanasaidia sana.

“Faida nyingine ya mafuta ya ufuta ni kuondoa maradhi ya ya ngozi, meno, na mifupa.Tafiti za kitaalamu zimebaini kuwa kula ufuta wenyewe unasaidia kulinda ini dhidi ya magonjwa,” ameweka wazi mtaalam huyo.
Aidha, amewataka wenye matatizo ya kiafya ya aina yoyote waende kupata huduma katika kituo chake cha kutolea huduma za afya Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au wampigie simu namba 0745900600.
