Usafiri wa Mwendokasi hautaweza kuendelea kwa muda nchini Tanzania kutokana na athari za maandamano yaliyotokea wakati wa maandamani.
”Vituo vingi vya Mwendokasi vimeharibiwa na kwa mantiki hiyo tunaendelea kuusitisha usafiri huu kwa njia ya morogoro road na …Mbagala yaani BRT 2,” amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila.

Chalamila amesema kuwa sababu msingi iliyopelekea kuchukuliwa kwa hatua hiyo ni kutathmini uharibifu uliotokea.
”…Tunajua kwamba mfumo wa ukataji tiketi na mageti pia yameharibiwa, na kwa mantiki hiyo inatupasa tuwe na muda wa kuweza kurudisha hali kama ilivyo.” Chalamila aliongeza.
Kutokana na hatua hiyo, Chalamila aliombaMamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), kutoa vibali vya muda mfupi kwa mabasi ya kawaida ili yaweze kutoa huduma katika njia hizi. Kwa Hisani ya BBC.
