Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeapa lazima imkamate Mwanaharakati wa Mitandaoni Mange Kimambi ambaye ni Mtanzania anayeishi nchini Marekani, kutokana na kile kinachoelezwa kuhamamisha na kuchochea vurugu zilizotokea nchini kuanzia Oktoba 29 mwaka huu Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) Hamza Johari amesema hayo muda mfupi baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan Novemba 05.2025 kuendelea kuongoza ofisi hiyo.
Amesema ni jambo ambalo halikubaliki kuona mtu mmoja tu anahamasisha uvunjifu wa amani nchini halafu baadaye tena
anarudi kutamba na kujiapiza kuwa lazima arejee, jambo ambalo amelitafsiri kuwa ni dharau ya kiwango kikubwa kwa serikali na nchi na kwamba jambo hilo halikubaliki
“Haiwezekani mtu mmoja amekaa nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, dada tu hata ukimuangalia appearance yake, anawaambia watu wakatanye hivyo na wanaenda kufanya kweli, halafu halafu imetokea anaanza kutamba anasema bado nitakuja kivingine, lazima tumkamate” -Hamza Johari
Amesema licha ya kwamba vyombo vya Ulinzi na Usalama linafuatilia suala hilo kwa namna yake na kama sehemu ya majukumu yao ya msingi, lakini ofisi yake pia ina wajibu wa makusudi wa kuhakikisha inashughulikia suala hil.
Akizungumzia athari zilizotokana na vurugu hizo, Mwanasheria Mkuu huyo wa Serikali amesema mali za watu binafsi na za umma zimeharibiwa ikiwemo gari la ofisi yake mwenyewe ambalo limechomwa moto huku dereva akikimbia ‘waandamanaji’
“Tumeona mali za watu binafsi zimeharibiwa, tumeona mali za umma including gari la Mwanasheria Mkuu wa Serikali, yaani gari la ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali libachomwa moto?, haiwezekani, nimeambiwa kwamba na gari yetu pia imechomwa moto dereva kakimbia, lakini Wanasheria sisi tuko mahiri, najuwa tu tutakuja na solution zuri, kule kwenye MTC kule tunataka tukafikiri namna fulani ili tuweze kuishauri serikali vizur, najuwa watu wa vyombo vya ulinzi na usalama
watafikiri kivyao, wao wana sehemu yao, lakini sisi hatuwezi kusema eti lile ni suala la kiusalama tu hapana, lile pia ni suala la kisheria, yaani sheria zimepuuzwa, zimevunjwa” -Hamza Johari
