Mkutano mkubwa wa kisiasa na kijamii juu ya mustakabali wa nchi, ulioitishwa Nairobi, nchini Kenya, na rais wa zamani Joseph Kabila, umezindua jukwaa jipya la kisiasa siku ya Jumatano, Oktoba 15, 2025, liitwalo “le Mouvement sauvons la République démocratique du Congo” (tuokoe Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo).
Kulingana na vyanzo vya ndani, mwishoni mwa mkutano, washiriki walimteua Joseph Kabila kama kiongozi wa vuguvugu hili.
Kwa mujibu wa tamko la mwisho la kongamano hili lililotolewa siku ya Jumatano, lengo la vuguvugu hili ni kuchukua hatua kukomesha udikteta na kurejesha mamlaka ya serikali.
Wapinzani hawa wameamua, hasa, kuidhinisha pointi kumi na mbili za kumaliza mgogoro wa DRC zilizopendekezwa na Joseph Kabila katika hotuba yake ya mwisho kwa taifa.
Kongamano hilo linataka kuwepo kwa mazungumzo jumuishi, yanayoungwa mkono na Baraza la Kitaifa la Maaskofu wa Kongo (CENCO) na Kanisa la Kristo nchini Kongo (ECC), kutatua mgogoro huo. Linakataa “mlolongo wowote wa kisiasa” uliopangwa, kulingana na washiriki, na Rais Félix Tshisekedi.
Ikumbukwe kuwa anakabiliwa na hukumu ya kifo iliyotolewa na mahakama ya kijeshi nchini DRC.
