Kiongozi wa mapinduzi wa Madagascar Kanali Michael Randrianirina ameapishwa ljana kuwa rais wa nchi hiyo. Ni baada ya jeshi kuchukua mamlaka katika taifa hilo la kisiwa mapema wiki hii kufuatia maandamano.
Kiongozi wa mapinduzi wa Madagascar Kanali Michael Randrianirina ameapishwa jana kuwa rais wa nchi hiyo, baada ya jeshi kuchukua mamlaka katika taifa hilo la kisiwa mapema wiki hii kufuatia maandamano yaliyoongozwa na vijana ambayo yalimlazimu Rais Andry Rajoelina kukimbia nchi.
Rajoelina, ambaye wabunge walimtimua baada ya kutorokea nje ya nchi mwishoni mwa juma, amelaani unyakuzi huo wa madaraka na kukataa kuachia madaraka licha ya uasi mkubwa katika vikosi vya usalama. Umoja wa Afrika (AU) na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) Antonio Guterres wamelaani mapinduzi hayo yaliyotokea baada ya wiki kadhaa za maandamano ya “Gen Z”.
Randrianirina alisema hapo awali kwamba jeshi lilichukua mamlaka na kuvunja taasisi zote isipokuwa Bunge la Kitaifa. Pia aliongeza kuwa kamati inayoongozwa na jeshi itatawala kwa hadi miaka miwili pamoja na serikali ya mpito kabla ya kuandaa uchaguzi mpya.
