Kesi ya mgawanyo wa mali namba 8323/2025 ya Chadema iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Zanzibar Said Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Bodi ya Wadhamini na Katibu Mkuu wa chama hicho, imeaanza kusikilizwa leo, Alhamisi Agosti 28.2025 Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam chiini ya Jaji Hamidu Mwanga
Ikimbukwe kuwa, katika kesi ya msingi Said Issa Mohamed na wenzake wanadai kuwa chama hicho kimekuwa kikiendesha shughuli zake pasipo kuzingatia usawa baina ya pande mbili ya Muungano yaani Tanzania Bara na Zanzibar, hali inayosababisha kuwa na mgao usiokubalika kisheria wa mali na raslimali fedha, huku ikidaiwa kuwa Zanzibar inapunjwa na haipewi kipaumbele katika mgawanyo huo
Sambamba na hilo, madai mengine yaliyowasilishwa Mahakama hapo ni kwamba baadhi ya kauli zinazotolewa miongoni mwa viongozi waandamizi wa chama hicho zimekuwa zikiashiria ubaguzi wa kidini jambo ambalo halikubaliki kwenye muktadha wa kisheria.Mandai TV iko Mahakamani hapo kukuletea kile kitakachojiri.
