Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika Wakili Boniface Mwabukusi amesema moja ya mambo aliyomueleza Rais Samia Suluhu Hassan alipokutana naye ni kuhusu mashtaka yanayomhusu Mwenyekiti wa @chadematzofficial Tundu Lissu @tunduantiphaslissu
Baada ya kukutana na Rais Samia janaAgosti 27, 2025 Ikulu jijini Dodoma Mwabukusi ameandika kupitia ukurasa wake wa X(Twitter) akisema “Suala la Mh. Tundu Lissu tuliliwasilisha kwake na linaendelea kuangaliwa na kufanyiwa kazi kwa utaratibu mwingine lakini bila kuingilia kinachoendelea Mahakamani”
Ikumbukwe Agosti 26, 2025 Mwabukusi alisema TLS inaiomba serikali kupitia Mkurugenzi Wa Mashtaka (DPP) kuziondoa kesi zinazomhusu Lissu ambaye kwa sasa anashikiliwa katika gereza la Ukonga kama mtuhumiwa wa mashtaka ya Uhaini, uchochezi na kuchapisha taarifa uongo kupitia mtandao wa YouTube.
Hata hivyo Mwabukusi ameeleza kuwa alipokutana na Rais Samia alimueleza mambo muhimu yanayohusu mustakabali wa Taifa ikiwemo masuala ya utekaji uwekwaji wa mifumo sawa ya uchaguzi ili kuwezesha uwepo wa ushiriki huru wa wananchi katika chaguzi mbalimbali nchini.