Jaji Mkuu mstaafu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma, amesema kuwa kuundwa kwa Tume Huru ya Uchunguzi wa matukio ya vurugu yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025 ni taswira nzuri inayoonesha kuwa nchi ina uwezo wa kushughulikia na kutatua changamoto zake yenyewe bila kuingiliwa na watu wa nje.
Prof. Ibrahim amesisitiza kuwa tume hiyo ni huru na haiingiliwi na taasisi au mtu yeyote, na kwamba ina hadhi ya kimataifa kwa kuwa inaongozwa kwa kuzingatia misingi ya sheria za kimataifa, si za Tanzania pekee.
Ameongeza kuwa tume hiyo imeundwa na wataalamu wabobevu wenye uzoefu wa kazi za kimataifa.
