Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata boti ya mwendo kasi iliyokuwa ikisafirisha shehena ya mirungi kutoka Mombasa, Kenya kuja Dar es Salaam.
Kamishna wa DCEA, Aretas Lyimo amesema operesheni hiyo iliyofanyika usiku wa kuamkia leo Aprili 14, 2026 katika eneo la Bagamoyo Mkoani Pwani ilifanikiwa kukamata viroba 18 vyenye zaidi ya vifurushi 1,000 vya mirungi.
Watu wanne wamekamatwa kuhusiana na tukio hilo, huku Lyimo akisema boti hiyo ilikuwa ikifuatiliwa kwa muda mrefu na ni sehemu ya mtandao mkubwa wa usafirishaji wa dawa za kulevya.
DCEA imeonya kuwa itaendelea kuchukua hatua kali dhidi ya wote wanaojihusisha na biashara hiyo na kuwataka wananchi kushirikiana kutoa taarifa.
