Youlou Mabiala Mwimbaji wa Franco Aliyeimba Kwa Kiswahi ‘Asumani’
Kuanzia siku zake za mwanzo akiwa na bendi ya kihistoria ya OK Jazz hadi kazi yake ya kujitegemea, Youlou Mabiala alijitofautisha kwa mashairi yenye kugusa hisia kwa undani na melodi zinazobaki akilini hata muda mrefu baada ya muziki kuisha. Aliimba wimbo uitwao Asumani kwa kiswahili kwa weledi mkubwa (Nenda You Tube ukausikilizze)
Akiwa pamoja na magwiji kama Franco Luambo, Simaro Lutumba, Josky Kiambukuta, na Madilu System, aliwakilisha ubora na roho halisi ya rumba ya jadi ya Kongo.
Mnamo tarehe 15 Agosti 2004, alipokuwa akitumbuiza jijini Pointe-Noire wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Kongo, Youlou alipata kiharusi jukwaani. Muziki ulisimama ghafla na umati wa watu ukanyamaza kwa huzuni. Ana sauti kalinzuri na ya kuvutia.
Tangu wakati huo, ameishi maisha ya utulivu kati ya matibabu na mapumziko, hasa katika eneo la Paris, ingawa baadaye alirejea nchini kwake.
Ingawa haimbi tena, sauti yake inaendelea kusikika ndani ya mioyo yetu hasa wanaofuatilia muziki wake. Huyu alimuoa binti wa bosi wake, Lwambo Lwanzo Makiadi (Franco).
