Mbuyu ni mti unaostawi kwenye eneo lenye mvua chache. Wakati wa ukame hupukutisha majani yake. Mmea huu hutoa maua meupe makubwa yaliyo matamu huku kipenyo chake hufikia milimita 200. Matunda ya mbuyu ni ya mviringo kama yai huku ukubwa wake ukiwa ni zaidi ya milimita 120.
Tunda hilo lenye ngozi ngumu, ndani kuna unga wenye rangi ya maziwa na mbegu ngumu zenye rangi nyeusi zikiwa na umbo mfano wa figo. Unga huu uliosheheni vitamini C ukichanganya na maji unapata kinywaji kitamu au ukichanganya na unga mwingine unapata dawa zinazosaidia kuondokana na matatizo mbalimbali ya kiafya.
Gome la mbuyu lina unene wa milimita 50 hadi 100. Majani yake hufanana na kiganja chenye vidole vitano hadi saba.
Kwa Tanzania mibuyu imeenea maeneo mengi ya mwambao wa Pwani katika mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani, Morogoro na Tanga, pia mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida, Tabora na Shinyanga.
MATUMIZI YA MBUYU
Kwa miaka mingi na katika sehemu mbalimbali mbuyu umekuwa ukitumika kama sehemu ya hifadhi.
Katika mbuyu unaweza kupata maji kwa kuwa una asili ya maji mengi. Majani yake hutumika kama chakula (mboga za majani) na unga wa tunda la mbuyu hutumika kama kinywaji na tiba lishe. Majani yake yamesheheni vitamini C, sukari na aina nyingi za madini.
~Kunufaika na faida zilizomo katika majani, pika majani haya kula kama mboga nyingine za majani.
~Kula mbegu zake baada ya kukaanga, au unaweza pia kutwanga na kupata unga ambao unaweza kutumia badala ya kahawa.
~Unga wa majani ya mbuyu pia umesheheni wanga, nyuzinyuzi (fibre), madini ya chokaa, na vitamini C, tumia kwenye maji moto au uji ulil mwepesi kila siku kwa muda wa siku 14-30.
Ikiwa una tatizo lolote la kiafya karibu katika kituo chetu cha kutolea huduma Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam.
Tunamjali kila mgonjwa na kumpa huduma stahiki. Katika kuhudumia wenye matatizo ya kiafya tunatumia tiba lishe na virutubisho asilia.
Ikiwa unahitaji ufafanuzi wa jambo lolote unaweza kuwasiliana na mtaalam Abdallah MANDAI kwa namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com
