Zipo sababu nyingi zinazochangia kinga za mwili wa binadamu kushuka, miongoni mwazo ni ulaji wa lishe duni.
Mtu anapokumbwa na tatizo la kushuka kinga za mwili anakuwa katika hatari kubwa ya kukumbwa na magonjwa mbalimbali.
Hata hivyo, baadhi ya watu unapozungumzia suala la kupungua kinga za mwili, mawazo yao yanawapeleka katika ugonjwa wa Ukimwi.
Kushuka kinga za mwili kunasababishwa na mambo mengi ikiwamo maradhi kama Kifua Kikuu (TB), na mkanda wa jeshi.
TB na mkanda wa jeshi ni maradhi ambayo yalikuwapo duniani miaka mingi kabla ya kugunduliwa ugonjwa wa Ukimwi.
Wakati huo wazee wetu walitumia bidhaa asilia kuchochea ongezeko la kinga za mwili.
Katika mahojiano na Mtaalam wa mimea tiba Abdallah Mandai alielezea bidhaa ambazo ukitumia kulingana na maelekezo ya utaona mabadiliko makubwa katika mwili wako au ndugu yako anayekabiliwa na tatizo hilo.
~Chukua ndizi mbivu tatu, parachichi tatu, mayai matatu ya kuku wa asili, maziwa freshi nusu lita na asali vijiko vya chakula vitatu.
~Changanya mchanganyiko huo kisha kunywa glasi moja asubuhi na nyingine jioni utaona mabadiliko makubwa ya kiafya katika mwili wako.
~Mchanganyiko huo utamkinga mtumiaji dhidi ya magonjwa mbalimbali lakini pia ngozi yake itakuwa na nuru licha ya kuwa ilishambuliwa na upele au majipu.
Ikiwa una tatizo lolote la kiafya karibu katika kituo chetu cha kutolea huduma Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam.
Tunamjali kila mgonjwa na kumpa huduma stahiki. Katika kuhudumia wenye matatizo ya kiafya tunatumia tiba lishe na virutubisho asilia.
Ikiwa unahitaji ufafanuzi wa jambo lolote unaweza kuwasiliana na mtaalam Abdallah MANDAI kwa namba 0745900600 au tembelea tovuti yetu kwa anwani ya www.dkmandai.com
