
Licha ya ladha yake chachu pilipili manga ambazo ni mbegu mviringo zenye rangi nyeusi, zina umuhimu mkubwa katika mwili wa binadamu.
Mtaalam wa virutubisho tiba, Abdallah Mandai, amesema pilipili manga zinaondoa gesi tumboni, kupunguza tindikali na ni kinga dhidi ya hatari ya kukumbwa na shinikizo la damu.
Mandai ameyasema hayo leo Aprili 5, 2022, jijini Dar es Salaam, na kuongeza kuwa pilipili manga pia ni kinga dhidi aina mbalimbali za maradhi ya saratani na zinazuia meno kuharibika.

“Pilipili manga pia ni msaada mkubwa kwa mwanamke ambaye ameshajifungua. Anywe uji uliowekwa pilipili manga unasaidia kuondoa uchafu unaobaki kwenye kizazi.
“Kiungo hiki pia kinalinda afya ya ngozi ya binadamu hususan ya kichwa na hivyo kuondoa tatizo la mba kichwani. Unaweza kutumia katika uji au mchuzi wa nyama,” amesema Mandai.
