Hatua hiyo inakuja baada ya jopo la Majaji watatu (3) wanaosikiliza kesi hiyo Mahakamani hapo wakiongozwa na Jaji Ndunguru kumaliza kusikiliza hoja za pande zote mbili (2) kufuatia mapingamizi yaliyokuwa yamewekwa na mshtakiwa Tundu Lissu, ambaye kwenye kesi hiyo anajitetea mwenyewe.
Majaji wengine katika kesi hiyo ni Jaji James Karanyemana na Jaji Fernand ambao ni wa mahakama kuu ya Tanzania.
Katika mapingamizi hayo ambayo yamesikilizwa Mahakamani hapo kwa siku nne (4) mfululizo kuanzia Jumatatu ya Septemba 08.2025, Tundu Lissu ameiomba Mahakama kuifuta kesi hiyo kutokana na kile alichosema kuwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ‘iliyosikiliza’ kesi hiyo katika hatua za awali haikuwa na mamlaka ya kisheria nk.
