Na: Mtaalam Mandai simu 0745 900 600
Je, ni kweli chips ni chanzo cha maradhi kama kisukari,Chips ni Nini?
Chips ni viazi mviringo vilivyomenywa, kukatwa na kukaangwa kwenye mafuta.
Chips kuku au chips mayai ni chips zinazoliwa pamoja na nyama ya kuku au mayai, mara nyingi ya kisasa (broiler na mayai ya kisasa) ili bei ibaki nafuu.
Kwa sababu ya gharama ndogo na kushibisha haraka, chips ni chakula kinachopendwa na wengi. Lakini bei nafuu hii inakuja kwa gharama ya kiafya kutokana na mambo yafuatayo:
Sababu Zinazohusiana na Athari za Chips
1. Matumizi ya Mafuta ya Bei Nafuu
Wauzaji hutumia mafuta kama ya pamba, alizeti, mahindi au soya kwa sababu ni rahisi kupata na bei yake ipo chini.
Mafuta hayo mara nyingi huchemshwa tena na tena kwa siku kadhaa, hadi kuwa meusi, jambo linalozalisha kemikali hatari mwilini.
2. Chips ni Kundi la Wanga
Viazi ni chakula cha wanga. Hivyo, unapotuhumu chips unasema pia kuhusu vyakula vingine vya wanga kama wali, ugali, mikate na mandazi.
Athari kuu za vyakula vya wanga vingi ni:
Husababisha mtu kula mara kwa mara (njaa hurudi baada ya saa 2–3).
Huongeza sukari kwenye damu kwa kiasi kikubwa na kwa haraka.
Mwili ukipokea sukari nyingi kila mara, insulini huzalishwa kupita kiasi, na hatimaye huchangia kisukari, shinikizo la damu, unene kupita kiasi, matatizo ya uzazi na upungufu wa nguvu za kiume.
3. Matokeo ya Sukari Nyingi Mwilini
Sukari ikizidi mwilini huunganishwa na chembe nyekundu za damu na kusababisha glycation, hali inayozalisha sumu zinazoitwa Advanced Glycation End Products (AGEs).
Hali hii huharibu mishipa ya damu na kusababisha matatizo mbalimbali: upofu, figo kushindwa kazi, vidonda sugu, kupoteza nguvu za kiume, na hatimaye kukatwa viungo.
Prof. Tim Noakes wa Chuo Kikuu cha Cape Town anasema:
“Mgonjwa wa kisukari hufariki si kwa sababu sukari haifiki ubongoni, bali kwa sababu mishipa yote ya damu inachakaa kutokana na sukari nyingi mwilini.”
Kwa maneno mengine: Mharibifu mkubwa ni sukari.
4. Ubaya wa Mafuta Yanayotumika
Mafuta ya mbegu (alizeti, mahindi, pamba, soya) ni ya kundi la polyunsaturated oils, ambayo hayastahimili joto la juu. Yakiwa yanakaangwa mara kwa mara huzalisha free radicals – sumu zinazochangia oxidative stress mwilini.
Matokeo yake ni magonjwa kama: pumu, saratani, matatizo ya hedhi, uchovu wa kudumu na kuzeeka mapema.
Kwa kupikia kukaanga, mafuta yanayostahimili joto ni: samli (ghee), siagi (butter), na mafuta ya nazi.
Hatari Nyingine
Kuku wa kisasa na mayai ya kisasa hutumika kwa sababu ya bei nafuu, lakini mara nyingi havina ubora wa lishe kama kuku wa kienyeji.
Vyakula vya bei rahisi mara nyingi vimepungukiwa virutubishi muhimu, hivyo hubaki vinashibisha tumbo lakini kuathiri mwili kwa muda mrefu.
Hitimisho
Chips ni sehemu ya kundi la vyakula vya wanga. Unapotuhumu chips pekee, kumbuka unazungumzia vyakula vyote vya wanga.
Tatizo si chips peke yake, bali ni namna tunavyokula vyakula vya wanga kupita kiasi, aina ya mafuta tunayopikia, na marudio ya kula chakula hicho.
Jamii inapaswa kuelimishwa juu ya matumizi sahihi ya wanga na mafuta salama, badala ya kutoa vitisho visivyoeleza ukweli kisayansi.
