In this June 15, 2019 file photo, Gen. Mohammed Hamdan Dagalo, the deputy head of the military council, salutes during a rally, in Galawee, northern Sudan. Dagalo, a paramilitary commander from Darfur widely known as Hemedti, has emerged as Sudan’s main power broker in the months since the military overthrew President Omar al-Bashir. As the military and protest leaders work to hash out a final agreement on the country’s future, Hemedti’s rise, and the growing resistance to it, could plunge the country
Kiongozi wa kundi la Rapid Support Forces (RSF) nchini Sudan, Mohamed Hamdan Dagalo, maarufu kama Hemedti, ameongoza kikao cha kwanza cha serikali yake baada ya kuapishwa kuwa mkuu wa serikali mbadala inayopingana na ile ya kijeshi iliyoundwa hivi karibuni na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan. Hatua hiyo imezua hisia mseto na inatarajiwa kuongeza zaidi hali ya sintofahamu na mgawanyiko wa kisiasa katika taifa hilo ambalo tayari linakabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Sherehe ya kumuapisha Dagalo ilifanyika licha ya upinzani mkali kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, ikiwemo Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na mataifa makubwa yanayosisitiza kuwa uundwaji wa serikali mbili tofauti unaweza kuzidisha mgogoro wa kisiasa na kijeshi unaoendelea Sudan. Wadau hao wa kimataifa wameonya kwamba hatua hiyo inaweza kuongeza mateso kwa raia wa kawaida ambao tayari wanakumbwa na hali mbaya ya kibinadamu kutokana na mapigano yanayoendelea tangu Aprili 2023.
Katika kikao hicho cha kwanza, Dagalo aliahidi kwamba serikali yake itajikita katika kuleta uwiano mpya wa kisiasa, kulinda maslahi ya wananchi na kurejesha amani nchini humo. Hata hivyo, wachambuzi wanasema uamuzi huo unaonekana zaidi kama mkakati wa kisiasa wa kuhalalisha nafasi ya RSF katika medani ya kimataifa na kudhoofisha serikali ya kijeshi inayoongozwa na al-Burhan.
Kwa sasa, Sudan imegawanyika wazi kati ya kambi mbili kuu zinazohasimiana: serikali ya kijeshi chini ya Jenerali al-Burhan na serikali mbadala ya Dagalo, hali ambayo inatishia kulizamisha taifa hilo kwenye mgogoro wa muda mrefu zaidi. Wakati huo huo, raia wa kawaida wanaendelea kuwa wahanga wakubwa, wakikabiliwa na njaa, ukosefu wa huduma za msingi na ukimbizi wa kulazimishwa.
