Baada ya watu wengi kusumbuliwa na tatizo la Koo kwa nyakati tofauti. Mtaalam Abdallah Mandai ametoa ufafanuzi wa namna ya kutibu ugonjwa huo na kuweza kupona kabisa.
Koo ni nini?
Ni mrija wenye mashimo, wenye misuli ndani ya shingo unaoanzia nyuma ya pia na kuishia juu ya miriha ya hewa(mrija wa upepo) na umio(mrija unapenda tumboni).
Koo hufanya kama njia ya hewa ya kuingia kwenye mapafu na chakula cha kioevu kuingia kwenye umio.
MAUMIVU KATIKA KOO.
Maumivu ya Koo Ni dalili ya hisia za kuhisi maumivu, ukavu au kukwanguliwa kwa Koo. Tatizo hili huwapata watu wengi Sana duniani.
Hii inaweza kupelekea kushindwa au kupata shida kumeza chakula, mate au kunywa maji.
TIBA YAKE.
Zipo njia nyingi za kutibu maumivu ya Koo ikiwemo kisayansi na kwa kutumia mimea tiba.
Na hapa tutaangazia njia ya kutibu tatizo la koo kwa kutumia mimea tiba.
MAHITAJI.
•Mbegu za Chia (Chia seeds) vijiko vitatu.
•Karoti 2
•Komamanga 1
•Tui la Nazi
NAMNA YA KUANDAA
•Chukua tui la Nazi pamoja na mbegu za Chia vichanganye kisha vichemshe mpaka mchanganyiko huo utakapokua umechanganyika vizuri.
•Chukua Komamanga na Karoti itengenezee iwe juisi kisha ichanganye na mchanganyiko wa tui la Nazi na mbegu za Chia.
MUDA WA MATUMIZI
•Kwa mchanganyiko huo ni wa matumizi ya siku moja kutwa mara tatu
•Tumia mchanganyiko huo kwa muda wa miezi miwili tu.
Kwa mawasiliano, changamoto, pamoja na maswali kuhusiana na Koo wasiliana na Mtaalam Abdallah Mandai kwa namba:
0745 900 600
