KWIKWI NI NINI?
Kwikwi hutokea pale upumuaji wako unapositishwa kwa kipindi kifupi. Kwikwi inaweza kutokea bila sababu yo yote.
Mtaalam Abdallah Mandai anasema kuwa “kwa kawaida kwikwi si kitu cha kusumbua sana, lakini kwikwi ikiendelea kwa muda mrefu ni ishara ya tatizo la kiafya”.
Hivyo basi, fanya yafuatayo kama huduma ya kumtibu mgonjwa anayesumbuliwa na kwikwi.
Hatua ya kwanza:
Chukua Jani la mgomba ambalo bado changa kisha pondaponda na ukamulie maji yake kwenye kikombe.
Hatua ya pili:
Chukua mpira(pipe) au fimbo ya Jani la mpapai, pitisha fimbo hiyo dirishanj ili unapomnywesha mgonjwa aliye ndani anywe kwa urahisi.
Hatua ya tatu:
Anza kumnywesha mgonjwa huyo kwa kumimina dawa hiyo kwenye fimbo ya Jani la mpapai au pipe ukiwa kwa nje na yeye awe anakunywa akiwa ndani.
Hatua ya nne:
Huku zoezi la kumnywesha linaendelea, mnyweshaji anatakiwa awe anamuita mgonjwa anayekunywa dawa ili awe anaitika huku anaendelea kunywa dawa.
Kwa muda wa siku mbili tu, mgonjwa huyo atapona.
ANGALIZO:
-Mgonjwa anatakiwa awe ndani na mnyweshaji awe nje.
-Muuguzi wa mgonjwa au mnyweshaji anatakiwa amnyweshe mgonjwa dawa kabla hajaenda haja ndogo ya asubuhi. Anapoamka tu amnyweshe.
Kwa mawasiliano, changamoto pamoja na maswali kuhusiana na namna ya kumuhudumia mgonjwa wa kwikwi ukiwa nyumbani, wasiliana na Mtaalam Abdallah Mandai kwa namba:
0745 900 600.
