
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya makatibu wakuu wa Wizara ya Elimu na Maliasili na Utalii.
Taarifa iliyotolewa jana Juni 16, 2022, na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Zuhura Yunusu imesema Dk. Francis Michael amehamishiwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii.
Pia Rais Samia amemhamisha Profesa Eliamani Sedoyeka kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.

