
Katibu Mkuu wa NATO, Jens Stoltenberg amesema Ukraine inahitaji uungwaji mkono wa haraka kwa sababu iko katika hali ngumu.
Ametoa kauli hiyo kabla ya mkutano wa kilele wa muungano huo mjini Brussels, nchini Ubelgiji.
Stoltenberg amesema nchi wanachama wa NATO zitaendelea kuipatia Ukraine silaha nzito na mifumo ya makombora ya masafa marefu.
Anasubiri kifurushi kipya cha msaada kuafikiwa na Kiev wakati wa mkutano huo.”Tunalenga katika kuimarisha misaada,” amesema.
