Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma jana, Agosti 22, 2025, imetupilia mbali shauri lililofunguliwa na Mchungaji Dkt. Godfrey Malisa aliyepinga uhalali wa Rais Samia Suluhu Hassan na mgombea mwenza wake, Balozi Dk. Emmanuel Nchimbi, kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Uamuzi huo umetolewa kufuatia mapingamizi yaliyowasilishwa na mawakili wa CCM, Fabian Donates na Alex Mgongolwa, waliodai kuwa hatua za kufungua shauri hilo hazikufuata taratibu za kisheria. Kwa mujibu wao, mlalamikaji alipaswa kuwasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa chama na si Mwenyekiti.
Awali, wakili wa mlalamikaji, Denis Maringo, amedai kuwa taratibu zilizingatiwa, akieleza kuwa mnamo Februari 2025, Dk. Malisa alimwandikia barua Rais Samia akipinga uteuzi wake kupitia CCM.
Baada ya pande zote kusikilizwa, shauri hilo liliahirishwa hadi jana, ambapo Mahakama Kuu imetupilia mbali malalamiko ya Dk. Malisa nakukukubaliana na mapingamizi yaliyowasilishwa na CCM
