
Mkazi wa kijiji cha Kitwai A, wilayani Simanjiro, mkoa wa Manyara, Danile Abraham (40), amefariki dunia baada ya kushambuliwa na nyati wakati akipeleka ng’ombe kunywa maji jirani na hifadhi ya taifa ya Tarangire.
Tukio hilo lililozua simanzi, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara, Limited Mhongole, akizungumza na waandishi wa habari jana Jumanne Agosti 16, 2022 amesema lilitokea Agosti 9, mwaka huu, kijijini hapo.
Kamanda Mhongole amewataka wananchi wanaoishi karibu na hifadhi za wanyama pori kuchukua tahadhari dhidi ya wanyama wakali ili kuepuka madhara yanayoweza kusababishwa na wanyama hao.
