
Mtaalam wa virutubisho tiba, Abdallah Mandai amesema kijiko kimoja cha karafuu kikichemshwa kwenye lita tatu za maji ni tiba ya kipindupindu.
Amesema maji hayo yachemke na kubaki lita moja na nusu, baada ya kupoa yachujwe na kutunzwa kwenye chupa safi.
Mandai ameyasema hayo leo Jumatano, Agosti 17, 2022 jijini Dar es Salaam ambapo ameelekeza mgojwa anywe vijiko vitatu vya mezani kila baada ya saa moja kwa wakati wa mchana na kwa usiku kila baada ya saa tatu, atapata nafuu na kupona kabisa.
Hata hivyo, Mandai amesema kwa aliye karibu na hospitali, kituo cha afya au zahanati ni vema awahi kupata matibabu kwanza.
Kipindupindu ni ugonjwa unaosababishwa na vijidudu wanaojulikana kama vibrio cholera ambao unaenezwa na inzi au maji yenye vijidudu wa ugonjwa huo.

Kwa kawaida kipindupindu kinashambulia sehemu ya chini za utumbo mdogo. Dalili za awali ni pamoja na kuharisha kawaida na ghafla kasi huongezeka huku kinyesi chake kikiwa na rangi kama ya maji yaliyooshewa mchele.
Mgonjwa hujisikia kizunguzungu, hutapika, huwa na maumivu makali ya tumbo, kujisikia kiu na kushindwa kutulia sehemu moja. Tiba yake ni rahisi hususan mgonjwa anayewahi tiba katika hatua za awali.
Hata hivyo, Mandai anasema kwa mwenye tatizo lolote la kiafya aende katika kituo chake cha kutolea huduma za afya Ukonga Mongo la Ndege, Dar es Salaam au awasiliane naye kwa namba 0745900600.
