
Mtangazaji wa Azam TV, Ahmed Ally, leo Jumatatu Januari 3,2022, ameteuliwa kuwa Ofisa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba (SC).
Kabla ya kutangazwa kuwa Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally, alikuwa mtangazaji wa Azam TV, na kabla ya hapo alikuwa mfanyakazi wa muda mrefu kwenye kampuni ya Sahara Media (Radio Free Africa na Star TV).
Ukurasa wa Facebook wa SC umeandikwa:
“Ni kijana mchapakazi, mwenye uhusiano mzuri na watu wa aina zote, mtanashati na kubwa zaidi mapenzi yake kwa Simba hayapimiki.
Ahmed Ally karibu kwenye klabu ya maisha yako kuwatumikia Wanasimba kama Ofisa Habari na Mawasiliano.
Kabla ofisa habari wa Klabu ya Simba alikuwa Hadji Manara ambaye alitimkia Klabu ya Yanga SC mwishoni mwa msimu uliopita.
