Wicknell Chivayo na mke wake, Lucy “Lulu” Muteke, wanatarajiwa kuzikwa leo, Alhamisi Oktoba 8, 2026, katika Makaburi ya Glen Forest Memorial Park jijini Harare, Zimbabwe, baada ya familia, ndugu, marafiki na maelfu ya waombolezaji kukamilisha maandalizi ya mwisho ya mazishi.
Wanandoa hao walifariki pamoja na watu wengine watatu katika ajali ya helikopta iliyotokea Septemba 30, 2026, katika eneo la Kudenga Farm, Marondera, takribani kilomita 70 mashariki mwa Harare.
Jana Jumatano, Oktoba 7, miili ya Chivayo na Lucy ilichukuliwa katika kituo cha kuhifadhi miili cha Doves Funeral Services katikati ya Harare na kupelekwa katika nyumba ya familia yao eneo la Gletwin, ambako iliwekwa kwa ajili ya waombolezaji kutoa heshima zao za mwisho kabla ya mazishi ya leo.
Msafara huo ulivuta umati mkubwa wa watu katika mitaa ya Harare, huku polisi wakifunga baadhi ya barabara kuu ili kuruhusu magari yaliyobeba miili hiyo kupita.
Maelfu ya watu walijipanga kandokando ya barabara, wengine wakiwa wamevaa mavazi meupe na wengine wakirekodi kwa simu zao.Maandalizi ya kuondoa miili ya marehemu hao katika kituo cha mazishi cha Doves Funeral Services, katikati ya Harare, yamekamilika huku ndugu, marafiki, waombolezaji na waumini wa dhehebu la Johane Masowe WeChishanu Apostolic wakikusanyika kwa wingi.

Polisi wamefunga baadhi ya barabara zinazozunguka eneo hilo, ikiwemo Union Avenue, ili kurahisisha usafirishaji wa miili na kudhibiti umati mkubwa wa watu.
Familia za Chivayo na Muteke zimeondoka Gletwyn kuelekea Doves huku maandalizi ya safari ya mwisho ya wanandoa hao yakiendelea.
Umati mkubwa wa watu umekusanyika kushuhudia kuondoka kwa miili ya Chivayo na Lucy, huku wengi wakifika kutoa heshima zao za mwisho.

Chivayo alikuwa akifahamika nchini Zimbabwe kutokana na shughuli zake za biashara na ufadhili, pamoja na maisha yake ya hadhi ya juu yaliyomfanya kuwa mtu anayefuatiliwa kwa karibu na umma.
Hali ya huzuni imetawala katika eneo la mazishi, huku familia, marafiki, washirika wa marehemu na waumini wakishiriki katika maombi na tafakari.

Ibada ya mazishi yafanyika
Baada ya shughuli za awali katika Doves, ibada ya mazishi ya Chivayo na Lucy imefanyika katika Olwen Crockery House.
Ibada hiyo imeongozwa na Vapostori kwa kuzingatia taratibu na mafundisho ya dhehebu lao.
Ndani ya ukumbi, ndugu, marafiki na watu mbalimbali mashuhuri wamekusanyika kushiriki katika ibada hiyo, huku nyimbo na maombi vikitawala shughuli za kuwaaga marehemu.

Nje ya ukumbi, waombolezaji wameendelea kuimba na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kuwaaga wanandoa hao.
Baadhi ya waombolezaji wameonekana wakirusha fedha barabarani, huku wengine wakiburudisha waliohudhuria kwa kuigiza baadhi ya mambo yaliyohusishwa na maisha ya Chivayo.
Mwili wa Wicknell Chivayo na mke wake, Lucy Muteke maarufu kama Lulu, unatarajiwa kuzikwa pamoja kesho, Alhamisi, Oktoba 8, 2026, katika Makaburi ya Glen Forest jijini Harare.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na familia za Chivayo na Muteke, shughuli za mazishi zinatarajiwa kuanza saa 8:00 mchana.
Familia, ndugu, marafiki na waombolezaji wanaendelea kutoa heshima zao za mwisho kwa wanandoa hao, huku maandalizi ya mazishi yakiendelea.


S
