
Mtaalam wa virutubisho tiba Abdallah Mandai amesema tango ni tiba anuai ya vidonda vya tumbo.
“Kula matango kunafaa katika kukabiliana na maradhi ya vidonda vya tumbo,” amesema Mandai leo Ijumaa Agosti 26, 2022 jijini Dar es Salaam.
“Tango pamoja na mambo mengine husafisha utumbo mwembamba na kuutibu. Linaondoa na kuzuia magonjwa ya ini, figo na koo.
“Kwa kawaida unapokula tango ni vema usilimenye maganda licha ya kuwa wakati mwingine baadhi ya matango huwa machachu kidogo, lakini hufaa zaidi unapokula na maganda yake.

“Tatizo la vidonda vya tumbo lisipochukuliwa kwa umakini mkubwa linaweza kusababisha saratani ya utumbo au ya koo.
“Ili kupata faida zitokanazo na tango, unaweza kutengeneza juisi au kulitafuna. Lioshe vizuri kabla ya kula au kutengeneza juisi.
“Manufaa mengine tango; sugulia uso kwa kipande cha tango na juisi yake kuuoshea, linaondoa chunusi na kuufanya uso uwe na mvuto,” amesema mtaalam Abdallah Mandai.
