Klabu ya Yanga Leo imeingia mkataba na kampuni ya BlackBird kutokea Rotterdam Uholanzi. Mkataba huo ni kwa ajili ya teknolojia ya Artificial Intelligence (Al).
Mfumo huo ni kwaajili ya kusaidia kukusanya taarifa za wachezaji wa Klabu ya Yanga huku Yanga ikiwa ndio klabu ya kwanza Afrika kuingia kwenye mkataba huo.
“Tunayofuraha kubwa sana kuwa mshirika wa kiteknolojia na klabu ya Yanga. Tumeichagua Yanga kwa sababu ni klabu kubwa sana Afrika. Tumevutiwa sana na mchakato wao a mabadiliko”
“Mfumo huu wa mabadiliko wa klabu umetupatia sisi fursa ya kufanya kazi na moja ya klabu ambayo inaendanana na kasi ya teknolojia” @thimvdweyden –
