
Matatizo ya kichefuchefu kisichokoma, kiungulia, maumivu makali katika chembe ya moyo yanaweza kutibiwa kwa mmea ujulikanao kama Mamakafa.
Mtaalam wa Virutubisho Tiba, Abdallah Mandai amebainisha hilo leo Desemba 29, 2021, jijini Dar es Salaam, wakati akifichua magonjwa mbalimbali na tiba zake huku akiuelezea ni mmea wenye maajabu makubwa kitiba.
“Ikiwa mgonjwa anashindwa hata kunyanyua kitu kinachokuwa mbele yake, tumia Mamakafa, inaondoa sumu ambayo mtu amelishwa na kikohozi.
“Pia inaondoa mwasho sehemu za siri unaowakwaza kinababa na mama, ” amesema.
Ameendelea “Chemsha mmea huo, maji yake oshea sehemu zenye mwasho, inaondoa chango la kumwaga, inarudisha hisia za tendo la ndoa zilizotoweka kwa kinababa.
Mamakafa ni moja ya mimea ambao kwa jina la kitaalamu unajulikana kama ‘mimosa pudica’ hapa nchini unafahamika na watalaamu wa tiba kuwa ni mmea wenye maajabu.
Unategemewa na matabibu wa tiba asili kufanyia mazindiko ya makazi ya wanadamu lakini pia kuganga magonjwa sugu yaliyoshindikana katika tiba za kisasa.

