
Mahakama ya juu ya Gambia ipetupilia mbali kesi iliyowasilishwa dhidi ya ushindi wa rais Adama Barrow kwa madai kuwa walioiwasilisha hawakuzingatia hatua za kisheria.
Barrow alishinda uchaguzi wa Desemba 4 kwa asilimia 53 ya kura zilizopigwa akifuatiwa na mpinzani wake wa karibu Ousainou Darboe kwa asilimia 28 ya kura, wakati wagombea wengine wawili wakipinga matokeo kwa madai kuwa kulikuwa na dosari kwenye vituo vya kupigia kura, bila kutoa ushahidi.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Chama cha Darboe United Diplomatic (UDP), kiliwasilisha ombi la kufutwa mchakato huo kwenye mahakama ya juu kwa madai kwamba halikufanyika kwa njia ya haki.
Hata hivyo, mahakama imesema chama hicho hakikuwasilisha malalamishi hayo ndani ya siku 5 kwa Barrow kama inavyohitajika kwenye sheria za Gambia.
