
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametanga siku ya mapumziko leo Ijumaa kwa ajili ya kuwaombea wahudumu wa afya pamoja na familia zilizoathiriwa na virusi vya corona.
Nchi hiyo ya Afrika Mashariki inakabiliwa na wimbi la pili la virusivya corona, jambo lililomsukuma rais kuweka amri ya kutotemebea na kufungwa kwa shughuli mbalimbali mapema mwezi huu.
Bunge la Uganda nalo limefungwa kwa muda kwa wiki mbili huku maofisa wakisema watu 100 katika bunge hilo walipatikana na maambukizi ya virusi hivyo.
Idadi ya vifo vilivyothibitishwa imeongezeka mara 10 katika kipindi cha siku 14, kulingana na wavuti wa Our Word in Data,
Chini ya asilimia mbili ya watu ndio waliopokea walau dozi moja ya chanjo ya virusi vya corona.
Wakati haya yakijiri , Uingereza imeiongeza Uganda katika orodha yake ya nchi ambazo raia wake wamezuiwa kusafiri kwenda nchini humo.
Ofisi ya mambo ya kigeni na Jumuia ya Madola (FCO) imesema kuanzia Juni30, Uganda itahamia kwenye orodha nyekundu ya kuingia Uingereza.
