
Watu wenye silaha wamewaua raia wapatao 100 wilaya ya mashambani Kaskazini mwa Burkina Faso karibu na mpaka na Niger.
Washambuliaji waliwalenga wanaume lakini walionekana kuwaachia wanawake na watoto katika wilaya ya Seytenga Jumamosi usiku.
Chanzo cha usalama na vyanzo vingine viwili vilisema wote wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina.
Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulizi lakini inaelezwa shambulizi hilo lilitokea katika maeneo ya mpakani ambako wanamgambo wanaohusishwa ni al-Qaida na Islamic State.
Takribani watu 3,000 waliokimbia shambulizi hilo wamewasili Dori mji mkuu wa Burkina Faso katika eneo la Sahel ambako mashirika ya misaada yapo kwenye eneo alisema ofisa wa eneo hilo ambaye aliomba jina lake lisitajwe.
Kulikuwa na taarifa tofauti kuhusu idadi ya vifo. Ofisa huyo wa usalama jana Jumatatu alisema takribani watu 100 walifariki dunia.
Chanzo katika eneo hilo ambacho hakikutaka kutajwa jina kilisema idadi ya watu waliofariki ilikuwa 165.
