
Wizara ya mambo ya nje ya Israel imesema waziri wake mpya, Yair Lapid, atakwenda Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), wiki ijayo kwa ziara ya kwanza kabisa ya mwanadiplomasia wa juu wa Israel katika taifa hilo la Ghuba.
Ziara ya Lapid inakuja baada ya mataifa hayo mawili kuanzisha uhusiano mwaka uliopita, katika makubaliano yaliyoratibiwa na utawala wa Donald Trump, ambayo yalikuwa ya kwanza kati ya makubaliano manne sawa na mataifa ya Kiarabu, yaliyokuwa yameitenga Israel kuhusiana na mzozo wake na Wapalestina.
Serikali mpya ya Israel na utwala wa Rais Joe Biden nchini Marekani wamesema wanayo matumaini ya kufikia makubaliano sawa na mataifa mengine ya kiarabu.
Wizara ya mambo ya nje ya Israel imesema Lapid atazuri UAE Juni 29-30, na atazindua ubalozi wa Israel mjini Abu Dhabi, na ubalozi mdogo mjini Dubai.
