
Umoja wa Mataifa umesema zaidi ya watu 100 wengi wao wakiwa wanawake wameuawa kwenye kambi moja nchini Syria katika kipindi cha miezi 18.
Taarifa iliyotolewa jana Jumanne na Umoja wa Mataifa imezitaka nchi kuwarejesha makwao raia wao.
Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Syria, Imran Rizi amesema kambi ya Al-Hol inazidisha hofu ya kutokuwa na usalama na watoto wanaokamatwa na kuhukumiwa maisha.
Al-Hol iliyoko Kaskazini-mashariki inadhibitiwa na Wakurd ilikusudiwa kuwa kituo cha muda cha kushikilia watu.
Hata hivyo, bado inawashikilia takribani watu 56,000 wengi wao wakiwa Wasyria na Wairaq ambao baadhi yao wana uhusiano na kundi la wapiganaji wa Islamic State ambalo liliteka maeneo mengi ya Iraq na Syria mwaka 2014.
Wengine ni raia wa nchi nyingine wakiwamo watoto na jamaa wengine wa wapiganaji wa IS.
Asilimia 94 ya wafungwa ni wanawake na watoto Rizi ambaye ametembelea Al-Hol mara kadhaa aliwaambia waandishi wa habari mjini Geneva.
