
Zaidi ya watoto milioni 10 ni miongoni mwa wale wanaokabiliwa na ukame mkali katika eneo la Pembe ya Afrika unaotishia uhai wao.
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, Unicef, linakadiria kuwa idadi hii ni milioni tatu zaidi ya ilivyokuwa miezi miwili iliyopita.
Wanasema kama fedha zaidi zikiingia na mvua kunyesha, eneo hilo linaweza kukabiliwa na “vifo vingi vya watoto”.
Mkurugenzi Mtendaji wa Unicef, Catherine Russell, ameiambia BBC kwamba ukame “dharura iliyosababishwa na hali mbaya ya hewa katika kipindi cha miaka 40”.
“Kuna umakini mkubwa unaotokana na mzozo wa Ukraine, inabidi tuwaonyeshe watu kinachoendelea hapa ili kuhakikisha wanaelewa ugumu uliopo.
Mvua zisiponyesha hakika watu hawatapona kwa sababu ziko chache hapa,” alisema.
Unicef inahitaji takriban dola milioni 250 kwa ajili ya msaada wa kibinadamu kwa nchi za Ethiopia, Somalia, Kenya, Eritrea na Djibouti.
