Wafanyabiashara watatu wamefariki dunia na wengine 36 kujeruhiwa baada ya lori walilokuwa wamepanda kwenda mnadani kuacha njia na kupinduka wilayani Handeni, mkoa wa Tanga.
Wafanyabiashara 11 hali zao zinasemekana sio nzuri kutokana na majeraha waliyopata, hivyo wanaendelea kupatiwa matibabu kwenye hospitali ya wilaya Handeni.
