
Mtaalam wa virutubisho tiba, Abdallah Mandai amewataka wenye tatizo la harufu mbaya mdomoni kutumia pera bichi kukabiliana nalo.
Amesema pera husaidia kuondoa harufu mbaya mdomoni na kuponyesha fizi zinazotoa damu.
Ameyasema hayo leo Jumanne Agosti 2, 2022, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumzia umuhimu wa matunda na manufaa yake kwa afya ya binadamu.
“Ikiwa eneo ulilopo hakuna mapera basi tafuna majani matatu ya mpera kila baada ya mlo wa asubuhi.
“Au kunywa juisi ya matunda na mbogamboga ni chanzo kizuri cha viini vinavyohitajika kukabiliana na tatizo hilo,” amesema.

Amefafanua kuwa mtu mwenye harufu mbaya mdomoni anahitaji kula vyakula vyenye viini vinavyosaidia kukabiliana na tatizo hilo.
Mandai amesema ni vema mgonjwa ahakikishe anakunywa juisi ya matunda au kula matunda yenyewe au juisi ya mbogamboga au kula mbogamboga zenyewe katika milo yote.
Hata hivyo, amesema mlaji wa matunda na mbogamboga ni vema ahakikishe yameoshwa vizuri kwa maji safi na salama na aepuke kuzipika mboga za majani kwa muda mrefu.
Amewataka wenye tatizo la kiafya kwenda kwenye kituo chake cha kutolea huduma za afya Ukonga Mongolandege, Dar es Salaam au ampigie namba 0745900600 iwapo anataka ufafanuzi wa jambo.
