Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, Ummy Mwalimu, ametoa wito kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo hilo kumuunga mkono Kassim Amari Mbaraka, aliyepitishwa na Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuwa mgombea wa ubunge wa Tanga Mjini,
Akizungumza leo Agosti 25, 2025 na waandishi wa habari Amesema wajibu wa Wanaccm ni kuheshimu maamuzi yanayofanywa na vikao vya ndani ya chama huku akisisitiza umuhimu wa kuvunja makundi ndani ya chama.
“Kwa sisi WanaCCM pale ambapo chama tayari kimefanya maamuzi ya kumteua mtu kuwa mgombea wa CCM katika uchaguzi wa vyombo vya dola, wajibu wetu sisi sote ni kuheshimu uamuzi huo. Ninawaomba sana ndugu zangu kumuunga mkono ndugu yetu Kassim Amari Mbaraka ambaye ameteuliwa na chama chetu kuwa mgombea wetu wa Jimbo la Tanga Mjini,” amesema Ummy
