Tume Huru ya Uchaguzi imetangaza rasmi tarehe ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kuwa ni Jumatano, Oktoba 29, 2025. Tangazo hili limetolewa wakati wa uzinduzi wa ratiba ya uchaguzi mkuu uliofanyika leo Julai 26, 2025, Jijini Dodoma.
Tume imesema kuwa hatua hii ni sehemu ya maandalizi makubwa ya kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa ufanisi, haki, na kwa wakati unaofaa. Watanzania wanatarajiwa kushiriki kikamilifu katika zoezi hili muhimu la kidemokrasia.
