Klabu ya Yanga imetangaza hatua kubwa ya mabadiliko ndani ya kikosi chake kuelekea msimu wa 2025/2026, kwa kuthibitisha kuachana rasmi na wachezaji wake nyota watano, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya maboresho ya kikosi hicho kuelekea mashindano ya ndani na ya kimataifa.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi kutoka klabuni, wachezaji hao hawatakuwa sehemu ya mipango ya kocha mpya Romain Folz, huku uongozi ukithibitisha kuwa tayari zoezi la usajili wa wachezaji wapya linaendelea kwa kasiWalioachwa ni pamoja na Aziz Kiii, Mkude, Chama, na wengine wawili ambao tutawataja tukithibitishiwa.
