
Spika wa bunge la Marekani, Nancy Pelosi, ametua katika kisiwa cha Taiwan licha ya kitisho cha China juu ya ziara hiyo.
Ndege iliyombeba Pelosi iliondoka Malaysia, na kutumia njia ndefu ili kuikwepa bahari ya kusini ya China.
Shirika la habari la Reuters halikuweza kuthibitisha mara moja iwapo Pelosi na wajumbe wengine wa Marekani walikuwa wameabiri ndege hiyo ya chapa SPAR-19.
Awali Pelosi mwenyewe hakuthibitisha iwapo atakitembelea kisiwa cha Taiwan chenye utawala wa ndani, na ambacho China inadai kuwa sehemu ya himaya yake.
Hata hivyo, baadhi ya vyanzo vimeliambia shirika la habari la Reuters kuwa spika huyo wa Marekani anatarajiwa kuwasili katika mji mkuu wa Taiwan, Taipei baadaye leo Jumanne.
Ndege hiyo iliondoka katika mji mkuu wa Kuala Lumpur majira ya alasiri na kuelekea mashariki mwa Borneo, katika safari iliyoepuka kupitia bahari ya kusini ya China.
