
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amemteua mbunge kutoka jimbo lenye utawala ndani la Jubaland, Hamza Abdi Barre, kuwa waziri mkuu mpya wa taifa hilo.
Barre mwenye umri wa miaka 48 anachukua nafasi ya Mohamed Hussein Roble ambaye uhudumu wake wa miezi 22 uligubikwa na migogoro baina yake na rais aliyeondoka madarakani, Mohamed Abdullahi Mohamed, hali iliyoitisha Somalia kuelekea katika vurugu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Mkuu Barre amesema amefurahi kuaminiwa na rais hatua ambayo inampa moyo wa kufanya kazi kwa nguvu zote.
Kiongozi huyo mpya amewahi kuhudumu katika nafasi za serikali na siasa kuanzia 2011 hadi 2017.
