
Rais Samia Suluhu Hassan amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Zambia, Edgar Lungu, wananchi wake na familia ya marehemu Keneth Kaunda kufuatia kifo cha mkongwe huyo wa kisiasa barani Afrika.
Kaunda ambaye ni Mwasisi wa taifa hilo, amefariki dunia jana Alhamisi Juni 17 wakati anapatiwa matibabu ya maradhi ya nimonia akiwa na miaka 97.
Taarifa iliyotolewa jana na watoto wake wa kiume, Panji na Kambarage Kaunda, ilithibitishia kifo cha baba yao kilichotokea katika hospitali ya kijeshi mjini, Lusaka.
Hali kadhalika Mama Samia ametangaza siku saba za maombolezo huku bendera zikipepea nusu mlingoti katika kipindi hicho.
Zambia na Bara zima la Afrika limepoteza mwamba imara uliosaidia kuchokea amani ya nchi hiyo na bara hilo kwa ujumla, Mungu aiweke pema peponi roho ya Keneth Kaunda.
