
Rais wa Marekani, Joe Biden, ana wasiwasi taifa lake kugawanyika katika vikundi viwili kati ya waliopigwa chanjo na wasiopigwa.
Amesema hataki kuiona nchi ambayo imegawanyika ambapo wapo wanaoishi bila hofu ya COVID na pengine pana anguko la kifo na magonjwa mabaya.
Biden alitoa kauli hiyo jana Jumatano wakati akitangaza juhudi mpya za chanjo ya corona na vivutio huku akibainisha kuwa kupata chanjo sio kitendo cha mrengo wa kisiasa ameongeza Biden.
Amefafanua kuwa uzalishaji wa chanjo hizo ulifanyika chini ya uongozi wa marais kutoka pande zote mbili hivyo amesema anahitaji kuwa na Amerika moja iliyoungana bila hofu.
Biden ameweka lengo la kuchanja asilimia 70 ya watu wazima nchini Marekani na chanjo walau moja ifikapo Julai 4, wakati nchi hiyo itaadhimisha Siku yake ya Uhuru.
Hadi sasa Wamarekani waliokwishapata chanjo ya Corona ni asilimia 63.
Pamoja na viwango vya chanjo ya COVID-19 kubaki, nyuma hususan katika jamii za wachache, Biden anapendekeza chanjo katika mpango wa maduka, ambayo inajumuisha vinyozi wa mitaa na wasusi wa nywele 1,000.
Wasusi hao na vinyozi watahudhuria mafunzo mwezi huu kuhusu chanjo ya corona na kisha kutoa mafunzo katika vituo vyao.
