
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linachunguza sababu ya vifo vya wapenzi Bunaza Manyanda (34), na Happiness Zakaria, vilivyotokea Juni 8, jijini Dar es Salaam.
Uchunguzi huo unafanyika ikiwa imepita siku moja baada ya Manyanda kudaiwa kumwua Happines kwa kitu chenye ncha kali na kisha kujiua kwa mchanyiko wa sumu ya kuua wadudu, vidonge vya flajiri na pombe eneo la Charambe kwa Mbiku, jijini Dar es Salaam.
Taarifa kutoka Jeshi hilo iliyotolewa jana Juni 9 inasema Manyanda alikutwa amefariki dunia wakati polisi ilipokwenda ili kumtia mbaroni baada ya kumwua Happiness.
