
Katibu Mkuu wa Jumuia ya Kujihami (Nato), Jens Stoltenberg ametoa mwito kwa Urusi kukubali ukaguzi wa kiwanda cha nishati ya nyuklia kinachodhibitiwa na Urusi cha Zaporizhzhya nchini Ukraine.
Katika kikao cha waandishi wa habari mjini Brussels, Ubelgiji, Stoltenberg amesema ni suala la dharura kwa Urusi kuruhusu Shirika la Kimataifa la Kudhibiti Matumizi ya Nishati ya Atomiki – IAEA na kuhakikisha vikosi vyote vya Urusi vinaondoka katika kiwanda hicho.
Mkuu huyo wa NATO amesema kukamatwa kwa kiwanda cha nishati ya nyuklia cha Zaporizhzhya na vikosi vya Urusi kunaweka kitisho kikubwa kwa usalama na kiwanda hicho kwa sababu kinaongeza hatari ya kutokea ajali ya nyuklia au tukio la nyuklia na kuhatarisha umma wa Ukraine, nchi jirani na jamii ya kimataifa.
