
Watanzania wanajukumu la kumwombea Rais Samia Suluhu Hassani ili aweze kufanikisha dhamana aliyopewa na Mungu ya kuiongoza nchi.
Nabii na Mwinjilisti wa huduma ya Waabudua Halisi, Emmanuel Njole ameyasema hayo jana Alhamis jioni, Agosti 25, 2022, Pugu Kisumu, jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na wanahabari.
“Tunajukumu la kumwombea Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuwa yeye ni lango la kupitisha vitu kwa ajili ya nchi na wananchi.
“Yeye amepewa na Mungu dhamana ya kufanya uamuzi kwa ajili ya nchi, hivyo lazima tuombe kwa ajili yake,” amesema.
Ameongeza kuwa Rais Samia yeye ni mwanadamu hivyo pamoja na mambo mengine aombewe ili awe na afya njema daima itakayomwezesha kufanikisha majukumu mazito ya kuliongoza taifa.
