
Askofu wa Kanisa la Penticostal Evangelist Fellowship of Afrika (PEFA), Samsoni Raphaeli ameitaka jamii kumwamini na kumtumaini Mungu anayewezesha kila jambo.
Baba Askofu Raphael wa Zoni ya Temeke, jijini Dar es Salaam, ameyasema hayo kwenye Ibada Maalum ya maombi na maombezi katika kanisa hilo lililopo Magole jiji Dar es Salaam.
Amesema Wakristo wengi wanayumbishwa na imani potofu kutoka kwa baadhi ya manabii wanaohubiri Injili kimaslahi ambao wanawahadaa kwa kutumia viambatanibisho kuwa ndivyo vitawasaidia kwenye kuondokana na shida mbalimbali.
“Bado wakristo wanaamini kutumia mafuta, wengine sabuni na vitambaa kuwa hivyo vitawasaidia, amewataka watulie walipo wafundishwe neno ambalo litawaweka huru.
Kanisa la PEFA ni miongoni mwa makanisa yasiyoamini maji, mafuta wala vitambaa bali linasimama kwenye neno la Mungu na kuwafundisha waamini wake kujua kweli iwe kweli na kila muumini kulijua neno la Mungu na kulisimamia.
