
Makamu wa Rais Dk. Philip Mpango amemwonya mkandarasi anayekamilisha uwekaji lami daraja la Nyeburu linalounganisha Chanika na Pugu, jijini Dar es Salaam kuwa akiendelea uchelewesha ukamilishaji atakiona cha moto.
Amesema serikali imekuwa ikitoa tenda kwa wakandarasi wa ndani kwa kuamini kuwa wanauchungu na nchi yao lakini hali hiyo inakatisha tamaa.
Ameyasema hayo hivi karibu wakati akipita eneo hilo kuelekea nyumbani kwake Chanika.
“Nawewe (anamwambia mkandarasi) unajua kuwa mvua ikinyesha watu wanakaa ng’ambo ile kule kusubiri maji yapungue wavuke kwanini mnafanya hivi,” amesema.
Amewataka Tanrods na Tarura kuwasimamia wakandarasi ili wamalize kazi kwa wakati.
