Hatimaye aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini kupitia tiketi ya chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mchungaji Peter Msigwa rasmi amejiunga na chama cha Mapinduzi CCM
Mchungaji Peter Msigwa ametambulishwa jana Juni 30,2024 katika kikao cha Kamagi kuu ya Halamshauri kuu CCM kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt Samia Suluhu Hassan jijini Dar es Salaam.
Awali kulikuwa na tetesi kwamba Msigwa atajiunga CCM hasa baada ya kutoa tamko zito baada ya kubwagwa na Joseph Mbilinyi katika uchaguzi wa mwenyekiti wa chadema Kanda ya Nyasa.
