
Mchungaji Prisca Mfaume wa Kanisa EAGT Buyuni, jijini Dar es Salaam, ameitaka jamii ya Watanzania kumtumainia Mungu katika kila tatizo wanalopitia hata linaloonekana haliwezekani machoni pa wanadamu.
Ameyasema hayo hivi karibuni jijini Dar es Salaam katika mazungumzo baina yake na wanahabari waliomtembelea nyumbani kwake.
“Ukimkimbilia Mungu hata ukiwa na changamo za aina gani anaweza kukuokoa, hata kama wameshakuchimbia kaburi,” amebainisha Mchungaji huyo.
Mchungaji Prisca ambaye alizaliwa katika familia ya Kiislamu ya Swala Tano, amesema aliugua ugonjwa wa ajabu na kupona kwa kuwa Mungu aliingilia kati.
